Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.

D-Type Viza ya Taifa

Ni wapi kwa kutuma maombi?

Unaweza kutuma kwenye ofisi ya Konsula - 15 Mtwara Road, Oysterbay, Msasani.

Je natakiwa kupeleka maombi kwa mikono?

Fomu ya maombi ya Viza lazima iwasilishwe kwa mikono. Misheni ya Diplomasia haipokei maombi yatumwayo kwa njia ya fax, barua za kawaida au barua pepe.

Namna gani ya kuomba miadi?

Unaweza kuomba miadi ya kutuma maombi ya viza kwenye mfumo wa e-konsulat, tarehe zipo katika utaratibu wa kawaida.

Kumbuka kutuma maombi ya viza kwa muda usiopungua wiki mbili kabla ya tarehe ya safari iliyopangwa.

Ni taarifa gani ninazozihitaji ili kuwasilisha?
  1. Fomu ya maombi ya viza iliyojazwa kupitia mfumo wa e-konsulat, iliyochapishwa na kusainiwa.
  2. Picha ya rangi yenye ukubwa wa cm 3.5x4.5. Picha lazima iwe:
  • Kali, yenye kitambaa cheupe kwa nyuma (back ground) na iliyochapishwa kwenye karatasi lenye ubora,
  • Mpya isiyozidi miezi 6 iliyopita,
  • Iliyochukuliwa usoni ikionyesha macho vizuri na uso kutoka pande zote mbili kutokea juu kwenda mpaka kwenye mabega, na uso ukiwa unaonekana kwa asilimia 70-80% ya picha yote. Picha inatakiwa ipigwe bila kuvaa kitu chochote kichwani.
  1. Pasipoti iliyotolewa ndani ya miaka, iwe halali mpaka angalau miezi mitatu kabla ya tarehe ya mategemeo ya kurudi na ikiwa na angalau na nafasi za kurasa mbili kwa ajili ya viza.
  2. Nakala ya ukurasa wa pasipoti wenye taarifa binafsi na picha.
  3. Bima ya afya iliyohalali kutumika katika nchi zote za Umoja wa Ulaya kwa kiwango kisichopungua EUR 30,000.
  4. Nakala ya hati ya kitambulisho kuthibitisha makazi yako ndani ya wilaya ya konsula uliyotumia maombi yako.
  5. Uthibitisho kwamba una namna ya kutosha ya kujikimu fomu iliyotolewa maamuzi na misheni:
  6. Uthibitisho wa makazi (kwa mfano mwaliko rasmi au booking ya hotel au nafasi).
  7. Hati ya uthibitisho wa lengo lako la kukaa Poland.

Nyongeza, wakati unatuma maombi ya viza kwa wadogo unatakiwa:

  • Kibali cha maandishi cha mzazi/wazazi wa mtoto kuomba viza kikiwa kimethibitishwa na mthibitishaji. Kama kuna mlezi mmoja, inatakiwa ithibitishwe na cheti cha kuzaliwa, maamuzi ya mahakama kama ulinzi wa wazazi haupo au cheti kifo cha mzazi mwingine.
  • Pasipoti orijino za wazazi na nakala (kopi)
  • Cheti cha kuzaliwa orijino na nakala (kopi)

Kama mtoto ameingizwa kwa wazazi au kwenye pasipoti ya mlezi wa kisheria, tafadhali wasilisha maombi tofauti ya viza. Viza itaingizwa kwenye pasipoti ya mzazi au mlezi wa kisheria.

Tafadhali kumbuka:

  • Lazima utume maombi yako ya viza kwenye ofisi ya konsula au konsula ya ubalozi idara ya konsula ya wilaya ya eneo la makazi yako.
  • Kwa kawaida taarifa za hapo juu zinatosha kwa mtu kupata viza, ingawa ofisa wa konsula anaweza kutaka taarifa Zaidi.
  • Tuma maombi ya viza sio mapema zaidi ya miezi mitatu kabla ya safari yako iliyopangwa.
  • Ofisa wa konsula anaweza, lakini haipaswi kuwa hivi, kumwalika mwombaji kwa mahojiano.
  • Viza ya D-Type inakuruhusu kukaa kwenye nchi nyingine za Schengen kwa siku 90 zozote za kipindi cha siku 180. Ina maanisha kwamba kisheria unaweza kukaa kwenye eneo la Schengen tu kama kukaa kwako kulikuwa na siku chache chini ya siku 90 kwa siku 180 zilizopita.
  • Viza ya D-type inafanya kazi kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.
  • Kupata viza hakukupi uthibitisho wa uhakika wa kuingia Poland-maamuzi ya mwisho huwa yanatolewa na Walinzi wa mipaka.
Inagharimu kiasi gani?

Ada ya maombi ya viza dola (USD) 86 keshi na huwa hairudishwa bila kujali maamuzi ya ofisa wa konsula.

Kuna muda gani wa kusubiri?

Maamuzi kusiana na kutoa viza yanafanyika ndani ya siku 15 za siku za kazi kutoka siku ya tarehe ya malipo ya ada maombi. Kama zinatakiwa kupitiwa kwa kina Zaidi, muda matarajio unaweza kuongezeka mpaka siku 30. Kwa dharura na kwa kesi zilizothibitishwa, maamuzi yanaweza kufanyika ndani ya siku tatu za kazi.

Namna gani ya kupata taarifa?

Baada kuwasiliana na ofisi, taarifa zinaweza kupatikana wakati wa masaa ya konsula.

Namna gani ya kukata rufaa?

Kama hukubaliani na maamuzi ya ofisa wa konsula, unaweza kuomba maombi yako ya viza yapitiwe tena. Lazama utume maombi kwaajili ya kupitiwa tena kwenye ofisi ambayo imetoa maamuzi ndani ya siku 14 tangu kupokelewa.

Ada ya maombi haya kwa suala hili ni USD 90.      

Baada ya kuwasiliana na mamlaka husika, maombi ya kuomba kurudiwa yanaweza kuwasilishwa wakati wa masaa ya konsula.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, raia wa nchi nyingine anaweza kutuma maombi ya viza kwenye ubalozi?

Ubaolzi unaweza kupokea maombi ya viza kwa raia na wakazi wa nchi zinazotumia ubalozi huu tu. Uthibisho wa makazi unaohitajika.

Unaweza kutuma maombi ya viza kwa barua ama barua pepe?

Hapana, maombi ya viza lazima yapelekwe na mtu baada ya kuomba miadi kwenye mfumo wa e-konsulat katika mtandao (www.e-konsulat.gov.pl).

Je, ninaweza kulipa kwa njia ya benki?

Hapana, ada ya konsula inaweza kulipwa kwa pesa taslimu tu. Tafadhali uje na kiasi kilichotimia katika dola (USD) tu.

Je, ninahitaji kutoa uthibitisho wa tiketi ya ndege?

Hapana, booking ya ndege ya kurudi inatakiwa na maombi ya viza. Viza itatolewa kwa kipindi chote ikiwa ni pamoja na tarehe ya kufanya booking. Ununuzi wa tiketi ya ndege unaweza kufanywa baada ya viza kutolewa.

{"register":{"columns":[]}}