Kwenda Nyuma

Habari

  • 05.12.2021
    Ulinzi wa afya ni mojawapo ya vipaumbele vya ushirikiano wa maendeleo wa Poland na nchi za Afrika. Ndio maana mwaka huu tunaendelea kufadhili mradi wa shirika la APOPO unaotekelezwa nchini Tanzania, unaojumuisha kugundua ugonjwa wa kifua kikuu kwa msaada wa panya wakubwa wa kusini.
  • 25.11.2021
    Kama sehemu ya kusherehekea Mwaka wa Chopin, tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2021, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam uliandaa tamasha la piano kwa ushirikiano na Ubalozi wa Ujerumani lililochezwa na mpiga kinanda mahiri wa Poland Jan Krzysztof Broja.
  • 12.11.2021
    Wakati wa tafrija ya sherehe za kuadhimisha miaka 103 ya kupata uhuru iliyoandaliwa katika bustani za ubalozi wa Jamhuri Poland jijini Dar es salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alisoma barua kutoka kwa Waziri SzymonSzynkowskivelSęk yenye kuwatakia kheri wanadiaspora wa Poland duniani na alikumbuka historia ya kurejesha uhuru.
  • 01.11.2021
    Siku ya Watakatifu wote ilikua ni hafla ya kuwakumbuka watu waliohamishwa kutoka Poland kutokana na Vita vya Pili vya Dunia nchini Tanzania. Balozi Krzystof Buzalski pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Utamaduni na Urithi wa Taifa waliweka shada la maua katika makaburi ya Tengeru, na wawakilishi wengine wa ubalozi walitembelea makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  • 29.10.2021
    Ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Filamu la Ulaya, lililoungana na Tamasha la Kimataifa la Filamu visiwani Zanzibar, Oktoba 29, 2021, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam uliandaa onyesho la filamu iliyoshinda tuzo. “Sweat” katika Taasisi ya Ufaransa iliyopo nchini Tanzania.
  • 22.10.2021
    Fenicha mpya za shule, magodoro pamoja na jiko, vifaa vya kufulia na uwanja wa michezo vitahudumia watoto wadogo kutoka Segerea hivi karibuni, Wilaya ya Dar es Salaam, pamoja na wafanyakazi wa shule wanaofanya kazi katika shule ya chekechea. Ununuzi wa vitu vya msaada wa Poland utawawezesha Masista Wamisionari wa Familia Takatifu kufungua hivi karibuni jengo jipya la Chekechea-Holy Family Day Care.
  • 09.10.2021
    Katika ratiba ya utendaji kazi wa msaada wa Kipoland, Ubalozi wa Jamuhuri ya Poland Dar es Salaam unawezesha hatua za shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kazi kwa manufaa ya kuboresha muingiliano wa kimaisha wa watu na tembo katika Bonde la Kilombero. Lengo ni kutafuta ufumbuzi katika eneo la mwingiliano wa kimaisha baina ya wanyama na jamii ya wenyeji, kwa kuzingatia tatizo linalosababishwa na upanuzi wa makazi ya watu na kilimo kwenye maeneo ambayo wanyama hao wapo, kwa mfano kando kando ya mipaka ya maeneo hifadhi.
  • 23.09.2021
    Basi jipya la kituo cha kulelea watoto cha St. Angel Day Care kilichopo Kurasini, Dar es Salaam, limenunuliwa katika mfumo wa mradi wenye kichwa kisemacho “kuongeza fursa za elimu kwa watoto kurasini kwa kusaidia vyombo vya usafirishaji” kwa wengine kutoka katika mfuko wa misaada wa Poland.
  • 20.09.2021
    Jumamosi Septemba 18, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam kwa mara nyingine ulijiunga na Siku ya Usafi Duniani nchini Tanzania.
  • 08.09.2021
    Balozi Krzysztof Buzalski na Konsul Piotr Kruze walikutana Septemba 8, 2021, kundi la wanafunzi wenye bahati kutoka Tanzania waliotunikiwa chini ya programu ya Banach, mpango wa pamoja wa Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Elimu na Sayansi na Wakala wa Taifa wa Poland wa ubadilishano wa Kitaaluma. Programu imeelekezwa kwa vijana kutoka katika nchi zinazoendelea ambao wangependa kuchukua masomo ya shahada ya udhamili nchini Poland.
{"register":{"columns":[]}}