Kwenda Nyuma

Habari

  • 16.07.2021
    Katika nusu ya kwanza ya Julai 2021, tulipata furaha kuwakaribisha kundi la wasanii wa Poland waliotumbuiza wakati wa mfululizo wa matamasha kama sehemu ya Tamasha la Pamoja Zanzibar, lililoandaliwa na Radek Bond Bednarz, msanii na mtayarishaji wa Poland, mwanzilishi wa Eklektik jukwaa la kitamaduni, linalojulikana kwa shughuli zake huko Wraclaw.
  • 28.06.2021
    Maendeleo yenye tija baina ya nchi zote mbili na matarajio ya kuimarishwa, katika nyanja zote mbili za kisiasa na kiuchumi, zilikuwa ni mada za ziara ya Naibu Waziri Paweł Jabłoński katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnano Juni 22 -24, 2021
  • 14.06.2021
    Tarehe 11 Juni, 2021 Balozi Krzysztof Buzalski alishiriki katika uzinduzi wa mrengo mpya wa kituo cha afya kinachoendeshwa na Shirika la Masista wa Kipolishi Elizabethan Maganzo mkoani Geita. Shukrani kwa mradi uliotekelezwa na Masista kwa ushirikiano na shirika la Redemptoris Missio, unaofadhiliwa na msaada wa Poland, iliwezekana kujenga na kuandaa kituo cha X-ray na ultrasound pamoja na ofisi za madaktari bingwa. Mradi huo ulitekekezwa kama sehemu ya kampeni ya Polonia kwa majirani na usaidizi wa Kipolandi kwa mskini zaidi walioathiriwa na janga la virusi vya korona.
  • 05.05.2021
    Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani za ubalozi wa Poland jijini Dar es salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alikumbuka historia ya Katiba ya Mei 3 na kusoma barua kutoka kwa Waziri Zbigniew Rau na kuwatakia Poles.
  • 03.05.2021
    Katiba ya Mei 3, 1791 (Sheria ya Serikali) ilipitishwa na Bunge la Poland (Sejm) Mei 3, 1791 ambalo lilikuwa katika kikao tangu 1788, ambayo katika historia ya Poland inajulikana kama Bunge la Miaka Minne au Bunge Kuu.
  • 20.11.2020
    Mnamo tarehe Oktoba 20, 2020 Mheshimiwa balozi alifika Baraza la Kiswahi la Taifa la Tanzania (BAKITA) kwa ajili ya kufanya mtihani wake. Baada ya mtihani aliweza kupata ufaulu wa juu yaani daraja la kwanza.
  • 23.10.2020
    Tunakualika kutazama filamu fupi kuhusu Poland.
  • 25.09.2020
    Mnamo Septemba 25, 2020 Ubalozi wa Jamuhuri ya Poland Dar es Salaam iliandaa onyesho la filamu ya "The coldest Game" kwenye ukumbi Alliance Francaise  na ufunguzi wa maonyesho ya "John Paul wa pili - Papa wa Mdahalo".
{"register":{"columns":[]}}