Habari
-
23.11.2023Ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Filamu la Ulaya, lililoungana na Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar, tarehe 3 - 23 mwezi Novemba 2023, filamu kutoka nchi 10 za Ulaya, zikiwemo Poland na Ukraine, zilionyeshwa.
-
11.11.2023Katika tafrija ya kuadhimisha miaka 105 tangu Poland kupata uhuru, ilioandaliwa katika bustani za Ubalozi wa Poland mjini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski aliwasilisha maonyesho ya "Wanawake wa Uhuru", wakati bendi ya wamisionari wa kimataifa iliimba nyimbo za Kipolandi. Pia havikukosekana vyakula vya Kipoland vilivyoandaliwa na Ubalozi.
-
01.11.2023Siku ya November 1, 2023, Balozi Krzystof Buzalski pamoja na wasaidizi wake walitembelea na kuweka maua katika makaburi ya Wapoland zilizopo eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ubalozi unatunza makaburi kwenye maeneo 6 nchini, yenye raia waliofuatana na jeshi la Jenerali Anders aliyewalisi Tanganyika mwaka 1942.
-
30.06.2023Kuanzia tarehe 19 hadi 24 Juni 2023, mwandishi wa habari mashuhuri Tanzania, Bw. Charles Makakala, alitembelea Warsaw, Lublin na Gdansk kama sehemu ya ziara ya utafiti iliyoandaliwa na ubalozi wa Poland nchini Tanzania. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kushuhudia mafanikio na maendeleo nchini Poland, misaada inayotolewa na Poland na Wapoland kwenda nchini Ukraine inayopigana vita dhidi ya Urusi, na kumwonyesha mbinu za taarifa potofu za Urusi. Pamoja na hayo, Bw. Charles Makakala aliona shughuli za makampuni ya Kipoland kutoka sekta ya teknolojia ya kisasa zinazovutiwa kushirikiana na Tanzania.
-
05.05.2023Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Mei na kufafanua zaidi kuhusu historia ya Poland na mafanikio ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.
-
26.04.2023Tunawataarifu waombaji wa visa kuwa tarehe 1 Mei ( siku ya wafanyakazi) na tarehe 3 Mei ( siku ya katiba) Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam utafungwa. Aidha, upande wa viza wa ubalozi utafungwa tarehe 5 Mei.
-
11.04.2023Msaada wa Ubalozi na Msaada wa Poland (yaani Polish Aid) kwenye sehemu ya kuishi kwa amani baina ya watu na tembo, maendeleo endelevu ya jumuiya za mitaa, pamoja na ujenzi wa huduma za kisasa ya zimamoto, zilikuwa ni mada ya mazungumzo kati ya Balozi Krzysztof Buzalski na timu ya walinzi wa hifadhi ya taifa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali katika Bonde la Kilombero.
-
15.03.2023Tarehe 15 Machi 2023, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ujerumani, uliandaa tamasha la piano lililochezwa na mpiga kinanda mahiri wa Poland, Jan Krzysztof Broja, pamoja na kuwasilisha maonyesho ya Kipoland-Kiukraine yaitwayo "Mama, sitaki vita!", sambamba na maadhimisho ya hivi karibuni ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
-
03.01.2023Hakutakuwa na rufaa ya visa mnamo January 6 na 13, 2023 (ijumaa)
-
21.12.2022Balozi Krzysztof Buzalski alitembelea Udzungwa na Bonde la Kilombero, ambako, ni sehemu ya ruzuku ndogo zinazofadhiliwa ndani ya Msaada wa Kipoland, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam umekuwa ukisaidia kwa miaka kadhaa shughuli za shirika lisilo la kiserikali la STEP kulinda bioanuwai ya Tanzania na kufikia hali ambapo watu na wanyamapori wanaweza kuishi pamoja bila migogoro. Hii ni moja ya changamoto za wakati wetu.