Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Kompyuta Mpya kutolewa kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea, Tanzania

10.12.2023

Wanafunzi wa shule za sekondari, ufundi, pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea, tayari wanatumia kompyuta zilizonunuliwa mwaka huu kupitia mradi uliotekelezwa kwa pamoja na kituo hicho na Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, ukiwa umefadhiliwa na msaada wa Polish Aid.

Segerea 12.2023_1

Wanafunzi wa Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea, Dar es Salaam, wanatoka katika familia zenye hali ngumu ya kiuchumi na pia wenye uwezo wa wasitani kutoka Dar es Salaam na mikoa jirani. Msaada mdogo kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Poland, uliyotengwa mwaka 2023 kwa ajili ya mradi wa "Kukuza elimu ya kompyuta kwa vijana na walimu Segerea" uliruhusu si ununuzi wa kompyuta na programu muhimu za kompyuta hizo tu, bali pia uandaaji wa mafunzo ya kompyuta kwa zaidi ya wanafunzi 100 na wafanyakazi wa kituo hicho.

Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi wa Ubalozi wa Poland huko Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka, alikutana na wanafunzi wanaonufaika na mradi huo. Wanafunzi hao watakuwa na fursa ya kuendelea na elimu ya programu za IT na nyingine za chuo kikuu, hasa ukizingatia kwamba katika mazingira mengi leo kompyuta zinatumika na ni sehemu muhimu ya elimu katika ngazi zote za elimu.

Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea kipo pembezoni mwa mji mkuu wa kiuchumi wa Dar es Salaam. Kinaendeshwa na mapadre wa Kifransisko kutoka Poland. Kimekuwa kikifanya kazi kwa miaka 15 sasa na ni taasisi kubwa ikusanyayo zaidi ya watoto 1,600 na vijana ambao wapo kwenye madaraja mbalimbali ya elimu ya shule, chekechea, kwanzia shule ya msingi, ufundi na sekondari. Mwaka 2017, mfuko wa Polish Aid ulitengwa na kusaidia katika ujenzi wa shule ya elimu ya ufundi, na mwaka 2018 shule ya chekechea iliyopo ndani ya kituo hicho.

Wahitimu wa kwanza wa Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea tayari ni wanafunzi wa vyuo vikuu na wenye mafanikio.

Picha (3)

{"register":{"columns":[]}}