Kwenda Nyuma

Kuimarisha Huduma ya Dharura nchini Tanzania kupitia Msaada wa Polish Aid

05.01.2026

Chini ya mradi uliyodhaminiwa na Polish aid, vifaa vya matibabu viliwasilishwa katika hospitali mbili za mkoa wa Dar es Salaam na vile vile kwa Kituo cha Mafunzo ya Madawa ya Dharura ya Tanzania-Poland na kuimarisha mfumo wa huduma ya dharura ya matibabu ya Tanzania.

Provision of medical equipment to Mwanyalamala Regional Hospital. Picture of the representatives of Mwanyalamala Hospital and representative from AKHS.

Mwishoni mwa 2025, kwenye mfumo wa mradi wa Msaada wa Polish aid “Kuimarisha Huduma ya Dharura nchini Tanzania”, vifaa maalum vya matibabu vilinunuliwa na kuwaslilishwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala na Hospitali ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo pia vilitolewa kwa Kituo cha Mafunzo ya Tiba ya Dharura ya Tanzania–Poland jijini Dar es Salaam. Uwasilishaji ulijumuisha vifaa vya matibabu ya oksijeni na uingizaji hewa, seti za usimamizi wa njia ya hewa, na zana za kimsingi za utambuzi.

Mradi huu ulitekelezwa kwa kushirikisha timu ya Huduma ya Afya ya Aga Khan (AKHST) na inaunda sehemu ya ushirikiano wa maendeleo ya Poland na Tanzania katika sekta ya afya. Dhumuni lake lilikuwa kuongeza uwezo wa wafanyikazi wa matibabu katika kujibu ipasavyo hali za dharura na kuboresha ubora wa huduma zinazotolewa kwa wagonjwa katika idara za dharura.

Mwaka ujao, watu watakaonufaika moja kwa moja na mradi huo ni wataalamu zaidi ya 100 wa afya, ambao wataimarisha ujuzi wao wa kitaaluma kupitia vifaa na mafunzo mapya, pamoja na wagonjwa zaidi ya 3,000 wa idara ya dharura katika hospitali za Mwananyamala na Temeke, ambao watanufaika na kuboreshwa kwa huduma ya matibabu.

Picha (5)

{"register":{"columns":[]}}