Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Kuonyeshwa kwa Makala ya “Ambassador of Remembrance” katika Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam.

29.01.2025

Katika kuadhimisha miaka 80 ya ukombozi wa Auschwitz na maadhimisho ya 20 ya Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Maangamizi Makuu (yaani International Holocaust Remembrance Day), Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam uliandaa onyesho la makala ya Ambassador of Remembrance (Balozi wa Kumbukumbu) iliyoongozwa na Magdalena Żelasko.

Screening of the Documentary “Ambassador of Remembrance” directed by Magdalena Żelasko at the Embassy of the Republic of Poland in Dar es Salaam

Makala hiyo inasimulia kisa cha Stanisław Zalewski, ambaye, mnamo Septemba 1943, akiwa na umri wa miaka 17, alikamatwa huko Warsaw kwa kujihusisha na vuguvugu la upinzani la Poland na kufukuzwa na kupelekwa katika kambi ya mateso ya Wanazi ya Ujerumani na kambi ya maangamizi ya Auschwitz-Birkenau kufanya kazi ya kulazimishwa. Baadaye alihamishiwa kwenda kwenye kambi za Mauthausen na Gusen I na II, ambapo wafungwa walikabiliwa na hali zisizo za kibinadamu na kulazimishwa kufanya kazi ya utumwa kwenye sekta ya silaha ya Ujerumani.

 

Watazamaji walipata fursa ya kusikia ushuhuda wenye nguvu wa Bw. Zalewski, ambaye - kama wahasiriwa wengine wengi wa ugaidi wa Nazi - alinyamaza kuhusu alichopitiavya kusikitisha kwa miongo kadhaa. Ilikuwa baada ya miaka arobaini ndipo alipoanza kuhadithia hadithi yake. Leo, akiwa na umri wa miaka 99, anaendelea kutoa ushahidi, akitumikia kama Ambassador of Remembrance wa ajabu. Makala hii ya Magdalena Żelasko inampa, kwa mara ya kwanza, fursa ya kuifikia hadhira pana na ujumbe wake.

 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wanachama wa bodi ya kidiplomasia, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, na jamii ya Poland. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Kaimu Balozi Katarzyna Sobiecka alisisitiza kwamba taswira za Auschwitz - zinazoashiria mateso na ukatili usiofikirika - hutulazimisha kutafakari juu ya matokeo ya kutojali na kunyamaza mbele ya dhuluma na kutumika kama ukumbusho wa hitaji la kusimama dhidi ya aina zote za ubaguzi, chuki na uonevu. Alisisitiza kwamba katika kukumbuka Auschwitz, tunakumbatia jukumu la pamoja la kujenga amani, kulinda walio hatarini zaidi, na kuhangaikia  ulimwengu ambapo “never again”(kamwe tena)  sio tu ahadi, bali ahadi inayotetewa na wote.

 

Wakati wa hafla hiyo, washiriki waliona maonyesho ya Polish Outstanding Women (Wanawake Bora wa Poland) ambayo inamshirikisha Antonina Żabińska - ambaye, pamoja na mumewe, walisaidia kuwaokoa waliotoroka kutoka Ghetto ya Warsaw – na maonyesho ya The Europe We Share (Ulaya Tunayoshiriki) , iliyoonyesha maadili ambayo Poland inashiriki na jumuiya pana zaidi ya Ulaya.

Picha (3)

{"register":{"columns":[]}}