Maadhimisho ya miaka 234 tangu kupitishwa kwa Katiba ya Poland tarehe 3 Mei nchini Tanzania.
13.05.2025
Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani za Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, mkuu wa ubalozi huo, Sergiusz Wolski, alikumbuka historia ya kupitishwa kwa Katiba ya Poland ya tarehe 3 Mei na kusisitiza uhusiano wa kirafiki kati ya Poland na Tanzania.
Hali nzuri ya mahusiano kati ya Poland na Tanzania pia ilisisitizwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo, ambaye pamoja na mambo mengine, alikumbuka kuongezeka kwa biashara kati ya nchi hizi mbili na miradi mingi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja katika nyanja ya afya na elimu, ambayo imekuwa ikitekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mingi sasa ikiwa sehemu ya Msaada kutoka Poland. Pia aliangazia maendeleo chanya ya mahusiano kati ya jamii ya Poland na Tanzania, hasa shukrani kwa ongezeko la watalii na wafanyabiashara wa Poland visiwani Zanzibar.
Sherehe hiyo ilikusanya wageni wengi na ilikuwa na muziki ya Poland na kimataifa, pamoja na vyakula. Wageni hao walikuwa ni wakilishi kutoka Serikali ya Tanzania, wanadiplomasia, wanadiaspora wa Poland na wahitimu wa vyuo vikuu vya Poland.
Ilikuwa pia ni fursa ya kuwasilisha kwa wageni waalikwa maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland kwa ushirikiano na Makumbusho ya Kitaifa ya Teknolojia huko Warsaw ya "Uvumbuzi za Poland ambazo Zilibadilisha Ulimwengu". Maonyesho yalionyesha mchango wa Poland kwenye urithi wa kiufundi na kisayansi ulimwenguni kwa kukumbusha kwamba vitu na vifaa vingi vinavyotumika leo au vimekuwa msingi wa maendeleo ya teknolojia, kama vile kamera ya filamu inayoshikiliwa kwa mkono, redio isiyo na waya, redio ya kupokea na kutoa habari, skrini ya LCD, kwa hakika, ni kwa sababu ya wanasayansi kutoka Poland.