Onesho la Makala ya Kihistoria ‘In the Rearview’ katika Ubalozi wa Jamhuri ya Poland, Dar es Salaam
27.02.2025
Kwa kuadhimisha mwaka wa tatu tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland huko Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Ubalozi mpya wa Ukraine nchini Tanzania, uliandaa onyesho la makalaya kihistoria ‘In the Rearview’, iliyoongozwa na Maciek Hamela. Tukio hili liliwalenga hasa wanadiplomasia na jamii ya wenyeji wenye shauku ya kufuatilia hali ya sasa nchini Ukraine.
Makala hii imetengenezwa na Maciej Hamela, ambaye, baada ya kuzuka kwa vita, alinunua gari la mizigo lililotumika na kusafiri hadi Ukraine kuwasaidia wale waliolazimika kuacha makazi yao. Kwa miezi kadhaa, aliwasafirisha wakimbizi huku akirekodi hadithi zao za kusikitisha. Gari lake likawa kimbilio la muda—mahali ambapo walipata muda wa kupumzika na kushiriki uzoefu wao. Makala hii inaonyesha uhalisia wa vita kwa njia ya kipekee, ya kweli na ya kugusa hisia. Ni simulizi kuhusu upotevu, tumaini, na mshikamano wa kibinadamu mbele ya janga.
Kama sehemu ya tukio hili, maonyesho ya Mama, Sitaki Vita yaliwasilishwa, yakionesha ushuhuda wa kushtusha wa watoto—waathiriwa wa sasa wa vita nchini Ukraine pamoja na wale waliopitia Vita vya Pili vya Dunia.