Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Siku za Utamaduni za Poland nchini Tanzania

21.08.2025

Kundi la nyimbo na ngoma za kitaaluma, Jedliniok, kutoka Wrocław lilitumbuiza Dar es Salaam kwa mwaliko wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland, kuwasilisha utamaduni na muziki wa Poland.

Jedliniok in Goethe Institut

Tarehe 20 na 21 Agosti, kwa mwaliko wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kundi la nyimbo na ngoma za kitaaluma la Chuo Kikuu cha Wrocław cha Sayansi ya Mazingira na Maisha - Jedliniok - lilitumbuiza Lido Slipway na Goethe-Institut, likionyesha uzuri wa dansi za kitaifa na kikanda za Poland. Mavazi ya rangi, muziki mtamu, kuimba, na kucheza vilifurahisha watazamaji, na hivyo kuzua shauku kubwa miongoni mwa jamii ya Wapoland na atazamaji wa Kitanzania.

Katika ziara yao nchini Tanzania, kundi hilo pia lilishiriki katika warsha za muziki na ngoma zilizoandaliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam pamoja na Chuo cha Muziki cha Action. Awali wasanii kutoka Jedliniok pia walitumbuiza Zanzibar na Mambo huko Lushoto Tanzania Bara ambapo walitoa matamasha na kufanya warsha kwa wananchi wa maeneo hayo wakiwemo watoto.

Kuleta kwa pamoja wanafunzi wa vyuo vikuu vya Wrocław, Jedliniok imekuwa ikikuza utamaduni wa Poland kwa zaidi ya miaka 50. Likiwa na zaidi ya matamasha 3,000 nchini Poland na nje ya nchi, kundi hili limeiwakilisha Poland mara kwa mara kimataifa.

Picha (20)

{"register":{"columns":[]}}