Kwenda Nyuma

Soma nchini Poland kupitia Udhamini wa NAWA Banach

08.04.2026

Wanafunzi kutoka Tanzania wanakaribishwa kuomba nafasi katika Mpango/Udhamini wa Banach NAWA, unaotoa ufadhili kamili wa masomo ya Shahada ya Uzamili (Master's) nchini Poland katika fani mbalimbali za kitaaluma. Maombi yapo wazi hadi tarehe 8 Mei (au hadi nafasi zote zitakapojazwa).

Banach poster

Lengo la Mpango

Mpango wa Banach NAWA unawawezesha wahitimu wenye vipaji kutoka nchi zinazoendelea kujiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili katika vyuo vikuu vya umma nchini Poland, kwa lugha ya Kipolandi au Kiingereza.

Mpango huu unasimamiwa na Wakala wa Taifa wa Poland wa Mabadilishano ya Kitaaluma (NAWA), kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje, kama sehemu ya ushirikiano wa maendeleo wa Poland.

Lengo lake ni kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi washirika kwa kuboresha elimu na sifa za kitaaluma za raia wake.

 

Faida za Mpango/Udhamini

  • Posho ya kila mwezi ya PLN 2,500
  • Msamaha kamili wa ada za masomo katika vyuo vikuu vya umma
  • Kozi ya maandalizi inayofadhiliwa na NAWA (kwa masomo ya Kipolandi)
  • Posho ya safari ya mara moja ya PLN 2,500
  • Fursa ya kusoma kwa lugha ya Kipolandi au Kiingereza
  • Kozi ya lugha ya Kipolandi na utamaduni (kwa wanafunzi wanaosoma kwa Kiingereza)

Mpango huu uko wazi kwa raia wa Tanzania wanaotaka kusoma Shahada ya Uzamili nchini Poland katika nyanja mbalimbali za masomo. Orodha kamili ya nchi zinazostahili inapatikana hapa.

 

Mwisho wa Maombi

Tarehe 8 Mei (au hadi nafasi zote zitakapojazwa).

 

Jinsi ya Kuomba?

Maombi lazima yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa NAWA:
https://programs.nawa.gov.pl/login

Nyaraka zinazohitajika ni pamoja na:

1.    Nakala ya pasipoti
2.    Cheti cha shahada ya kwanza au uthibitisho kutoka chuo kikuu
3.    Uthibitisho wa kuomba katika chuo kikuu cha Poland
4.    Cheti cha umahiri wa lugha
5.    Video ya kujitambulisha (dakika 1–3, kwa lugha ya kiingereza)

Kwa Mawasiliano na Msaada

Barua pepe: banach@nawa.gov.pl

Simu: +48 451 058 642, +48 451 058 644

Maelezo zaidi: https://nawa.gov.pl/en/students/foreign-students/the-banach-scholarship-programme

Picha (1)

{"register":{"columns":[]}}