Tayari tunawafahamu washindi wa Mashindano ya Mdahalo wa Vijana wa Umoja wa Ulaya, ambao watasafiri kwenda Poland kama zawadi ya ushindi
31.01.2025
Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam ulikuwa mshirika mkuu wa Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya ulioanzishwa na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam, fainali ambayo ilifanyika Ijumaa iliyopita, Januari 31, 2025. Washindi wa shindano hilo walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu viwili vya Tanzania: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini.
Hapo awali washindani zaidi ya 400 waliomba kushiriki katika shindano. Kutoka kundi hili, washiriki 100 walichaguliwa kujiunga na mdahalo kwenye mitandao ya kijamii ulioanza Desemba 15 hadi 30, 2024. Katika hatua hii, washiriki 20 wa fainali walichaguliwa, ambao walishikiri na midahalo ya moja kwa moja kwenye Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar. es Salaam Januari 30-31, 2025. Timu nne zilizojumuisha wachezaji watano zilichuana kwa siku mbili, kuonyesha utamaduni wa juu wa midahalo, ujuzi wa hali ya juu wa kuzungumza mbele ya watu na ustadi wa kujadiliana.
Shindano hilo lilikuwa na hatua kadhaa, zikiwemo za mtandaoni na fainali zilizofanyika moja kwa moja jijini Dar es Salaam. Mada yake kuu ilikuwa mjadala ambao jinsi gani mtu anahakikisha mapato endelevu zaidi: kupitia kampuni binafsi/kujiajiri au ajira ya kutwa nzima. Shindano la Mdahalo wa Vijana wa Umoja wa Ulaya lilitangazwa tarehe 18 Novemba 2024, kama sehemu ya juhudi zilizofanywa na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na ujumbe wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya uliopo Tanzania, ukiwemo Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kuongeza ushiriki wa vijana wa Kitanzania katika mijadala ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi yao na kuboresha nafasi zao katika jamii. Ushindani wa mdahalo pia unakusudiwa kuboresha ustadi wa kufikiria kwa kina, mabishano yenye mantiki, ushirikiano na mawasiliano madhubuti. Zaidi ya hayo, inasaidia mijadala kuhusu masuala ya maendeleo na, zaidi ya yote, kuhimiza vijana kushiriki kwa kina zaidi katika changamoto za kijamii na kiuchumi za Tanzania na wakati huo huo kuboresha ujasiriamali wao, ambao pia unaendana na vipaumbele vya ushirikiano wa maendeleo wa Poland na Tanzania.
Zawadi katika shindano hilo zilitolewa kwa washindani binafsi na timu. Timu iliyoshinda ilipokea zawadi za fedha taslimu zilizodhaminiwa na Ujumbe wa umoja wa ulaya jijini Dar es Salaam.Kilichoamsha hisia nyingi 5ya washiriki na watazamaji, ilikuwa tuzo ushini ya ziara ya kielimu na kitamaduni nchini Poland, ambayo itafanywa wakati wa msimu wa kiangazi baadaye mwaka huu kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam.
Fainali ya shindano hilo katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilikusanya watazamaji zaidi ya 400, wakiwemo wanafunzi, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, viongozi wa sekta binafsi na wawakilishi wa vyombo vya habari. Pia, ilivutia watazamaji wengi kufuatia utiririshaji mtandaoni wa fainali. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya Christine Grau na Kaimu balozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka. Katika hotuba yake, Mkuu wa Ujumbe wa umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam alisisitiza umuhimu wa kukuza fikra makini miongoni mwa vijana na kubainisha kuwa Umoja wa Ulaya unajivunia kuunga mkono mipango hiyo. Pia alionyesha matumaini kuwa tukio hili linaweza kuwa la kila mwaka na kuwafikia wanafunzi wengi zaidi na kuchangia kuimarisha utamaduni wa midahalo nchini Tanzania. Akiwahutubia washindani, majaji na watazamaji waliokusanyika katika fainali ya shindano hilo, Mkuu wa Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka alielezea kufurahishwa kwake na ubora wa mdahalo huo ambao ulifanyika kwa kuheshimu maoni ya wapinzani. Ubora huu bila shaka ulitokana na vipaji na maandalizi mazuri ya kiufundi na ya kina ya washiriki. Katarzyna Sobiecka pia aliangazia ushiriki wa muda mrefu wa Poland katika kusaidia maendeleo na kuwawezesha vijana wa Tanzania, hasa ndani ya mfumo wa ushirikiano wa kimaendeleo na miradi inayotekelezwa kupitia ufadhili wa Polish Aid. Katarzyna Sobiecka aliwapongeza washindi wote, hasa wale waliopata idadi kubwa zaidi ya pointi na hivyo kushinda ziara ya elimu na utamaduni nchini Poland iliyofadhiliwa na Poland, yaani, Bibi Careen James Ndika (Shahada ya Sayansi katika Sayansi ya Actuarial, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Diana Shabani (Shahada ya Sheria, Chuo Kikuu cha Tumaini) na Kijafaraja Maduhu (Shahada ya Sanaa katika Masomo ya Mawasiliano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).
Chargée d'affaires a.i. wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka alienda kusema, ”Tunawapongeza kwa ushindi wao na tunatumai kwamba ziara yao nchini Poland itawawezesha kupata marafiki wapya, wa kupendeza, kukuza ujuzi wao wa historia, jiografia, utamaduni, usanifu, sanaa na vyakula vya Poland, na pia kuleta karibu uzoefu wa Kipolandi. kuhusiana na mafanikio ya mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika miongo michache iliyopita, hasa tangu Poland kujiunga katika Umoja wa Ulaya. Vitabu vinavyoitwa About Polska vilivyopokelewa na washindi kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam hakika vitawasaidia kujiandaa kwa safari yao ya Poland.”
Picha: Ujumbe wa Umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam / Bw. David Masanja