Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Timu ya Wanahistoria kutoka Kraków Yarejesha Hali ya Makaburi ya Poland huko Kondoa

09.02.2025

Makaburi ya Kondoa yalikuwa eneo la mwisho ambapowamezikwa Wapoland nchini Tanzania linalohitaji urejesho wa kina wa hali.

Kondoa

Makaburi ya Kondoa yanatumika kama mahali pa mwisho pa kupumzika kwa Wapoland waliofukuzwa kwao kwenda ndani ya USSR (Muungano wa Sovieti) baada ya kuzuka kwa Vita Kuu ya pili ya Dunia. Mkataba wa Sikorski-Mayski umewawezesha kuondoka katika maeneo yao ya uhamisho na mwaka 1942, walifikia makazi ya wakimbizi huko Afrika. Mojawapo kati ya makazi sita ya Wapoland katika Tanzania ya leo (wakati huo Tanganyika ya Uingereza) ilikuwa Kondoa, nyumbani kwa takriban watu 430, kati ya 1942 na 1948.

Licha ya hali ngumu ya mvua kubwa, kukatika kwa umeme, na maua ya mbuyu ambayo yalichafua mawe ya kaburi yalipoangukia, kazi ya ukarabati ilikamilika ndani ya wiki mbili tu. Mawe ya awali yaliofunika makaburi ya wahamishwa wa Siberiakwa mtindo wa kienyeji, yalirejeshwa katika muonekano wake wa awali.

Kazi ya uhifadhi na urejeshaji katika makaburi hayo ilisimamiwa na Prof. Hubert Chudzio wa Taasisi ya Historia na Mafunzo ya Nyaraka katika Chuo Kikuu cha Tume ya Kitaifa ya Elimu (UKEN), ambaye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha Nyaraka za Uhamishaji, Kufukuzwa na makazi mapya.

Mradi huo ulifanywa kwa ushirikiano wa Wizara ya Utamaduni na Urithi wa Kitaifa wa Poland, Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, na tasisi ya ‘’The Past Does Not Return but It Does Not Die" (yaani, „Yaliyopita Hayarudi Bali Hayafi”).  Fedha zilitolewa na Wizara ya Utamaduni na Urithi wa Taifa kupitia Mfuko wa Kukuza Utamaduni.

Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, kwa msaada wa fedha za diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland, pia ulifadhili uchapishaji na ufungaji wa ubao mpya wenye taarifa kwenye makaburi ya Poland yaliyopo Bigwa karibu na Morogoro. Ubao hizi ziliwekwa na wanahistoria wa Kraków walipoelekea Kondoa.

Wakati wa misheni yao nchini Tanzania, wakiungwa mkono na Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, wanahistoria hao pia walitembelea Hifadhi ya Nyaraka ya Taifa ya Tanzania jijini Dar es Salaam, ambako walifanya utafiti kuhusu nyaraka zinazohusiana na makazi ya Poland katika Tanganyika ya zamani. Walipokelewa kwa vizuri katika Ubalozi wetu, ambapo majadiliano yalifanyika kuhusu shughuli za sasa na zilizopangwa za Kituo cha Nyaraka katika Bara la Afrika.

Picha (10)

{"register":{"columns":[]}}