Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Tumeshiriki katika Mradi wa EUNIC "Viraka Freshi" nchini Tanzania

01.03.2024

Kama sehemu ya ushirikiano na EUNIC (Taasisi za Kitaifa za Utamaduni za Umoja wa Ulaya) nchini Tanzania, tulishiriki katika utekelezaji wa mradi wa "Viraka Freshi/Vipande Vipya", unaounga mkono vijana wabunifu wa Kitanzania katika sekta ya uzalishaji wa chapa mbalimbali na endelevu za kimitindo. Washirika waliounga mkono mradi ni mabalozi ya: Ufaransa, Hispania, Ujerumani, Italia, Ireland, Poland na Umoja wa Ulaya - EU, pamoja na mashirika ya Alliance Francaise, Goethe Institut na British Council, na pia mashirika ya ndani ya nchi kama vile Naledi Creative Center na CDEA Fashion Incubator.

Viraka Freshi Fashion Show 2024_0

Wakilishi wa ubalozi walishiriki katika Onyesho la Mitindo la Viraka Freshi, ambalo lilikuwa ni kilele cha mradi huu wa miezi kadhaa, ambao ulifanyika tarehe 1 Machi 2024 katika Taasisi ya Alliance Française. Maonyesho yalikuwa ya mtindo endelevu iliyotumia mchanganyiko wa kipekee vya vitambaa vilivyotumika. Onyesho hilo lilivutia watazamaji wengi pamoja na vyombo vya habari.

Onyesho la mwisho la mitindo lilitanguliwa na wiki 8 za warsha kwa washiriki wabunifu 11 kutoka Tanzania. Katika muda huo, Viraka Freshi Incubator iliwapa washiriki vikao vya ushauri kukuza ujuzi wa kushona, kama vile utumiaji wa mashine za kitaalamu, ubunifu, mbinu za kufunga na kuchapa rangi, na pia uuzaji.

Picha (8)

{"register":{"columns":[]}}