Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Ubalozi wa Poland jijini Dar Es Salaam kama mshirika mkuu wa mradi wa mashindano ya mdhahlo ya vijana ya Umoja wa Ulaya

30.01.2025

Chargée d'affaires a.i. wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam Katarzyna Sobiecka alizungumza na ‘The Chanzo’ kuhusu mahusiano ya Poland na Tanzania na ushiriki wetu katika Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya. Fedha za Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland na Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam zimewezesha washindi watatu wa juu wa Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya watazuru Poland mwaka huu!

Interview for the Chanzo

Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam ulikuwa mshirika mkuu wa mradi wa Mashindano ya Mdahalo ya Vijana ya Umoja wa Ulaya ulioanzishwa na kufadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam. Fainali za shindano hili la midahalo zilifanyika moja kwa moja katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Januari 30-31, 2025. Washindi wa shindano hilo walikuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu viwili vya Tanzania ambao kila mmoja alipata alama nyingi zaidi wakati wa mdahalo: Bi. Careen James Ndika na Kijafaraja Maduhu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Bibi Diana Shabani kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini. Kwa mara nyingine tena, tungependa kuwapongeza washindi hao kwa kutunukiwa tuzo la ushindi ya ziara ya kielimu na utamaduni nchini Poland, iliyofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, ambayo itafanywa wakati wa majira ya joto baadaye mwaka huu.

Tunakualika usikilize mahojiano mafupi na mkuu wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka na The Chanzo, mmoja wa washirika wa mradi huo, kuhusu sio tu ushiriki wa Poland katika Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya, lakini pia kuhusu uhusiano wa Poland na Tanzania.

 Video: The Chanzo

Video

{"register":{"columns":[]}}