Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya

10.12.2024

Mazungumzo ya kwanza ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya chini ya Mkataba wa Samoa yalifanyika tarehe 10 Desemba 2024 jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo ya Ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya - Tanzania 10 Desemba 2024 picha ya pamoja

Mazungumzo ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) ulilenga mada kama vile: mahusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania kwa kuzingatia makubaliano mapya ya Samoa, utawala bora na demokrasia, ushirikiano katika nyanja ya uchumi na ukuaji endelevu (ikiwa ni pamoja na uwekezaji na sekta binafsi, biashara, mkakati wa Global Gateway, mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi wa bluu), usalama wa baharini, kupambana na itikadi kali, ugaidi na uhalifu uliopangwa (Umoja wa Ulaya tayari umekuwa ukifanya kazi kwenye kanda kwenye eleo la usalama wa baharini, kupambana na uhalifu wa kupangwa na kuboresha taratibu za kukabiliana na utakatishaji fedha), pamoja na hali ya usalama ya kimataifa na nafasi ya Tanzania kikanda katika Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) na  Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC).

Wakati wa mazungumzo, uhusiano imara wa Umoja wa Ulaya na Tanzania uliojengwa juu ya miongo ya maadili na maslahi ya pamoja, ushirikiano, ushirikiano na urafiki, ulithibitishwa tena. Pande zote mbili zilithibitisha dhamira ya pamoja ya kuheshimu haki za kimsingi na uhuru, pamoja na maadili ya kidemokrasia, utawala bora, na uhusiano wa amani wa kimataifa kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu.

Wakati wa kujadili ushirikiano wa kiusalama, Umoja wa Ulaya ulipongeza mchango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta utulivu katika Ukanda wa Maziwa Makuu na Kaskazini mwa Msumbiji, na kuzingatia  ombi la kwanza la Tanzania la msaada chini ya Kituo cha Amani cha Ulaya ili kufanikisha mipango yake ya amani na usalama.

Umoja wa Ulaya na Tanzania pia zilisisitiza dhamira ya pamoja ya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi na kubainisha maendeleo katika kusaidia ukuaji endelevu na utulivu wa kikanda. Umoja wa Ulaya ulikumbuka kuwa kwa ujumla wake umekuwa mwekezaji mkubwa nchini Tanzania, hasa katika sekta za nishati, utalii, kilimo na miundo mbinu. Mwaka jana, watalii wengi waliotembelea nchi hii, hasa Zanzibar, walikuwa ni raia wa Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya na nchi wanachama pia ni wawekezaji wakubwa katika sekta binafsi Zanzibar. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Umoja wa Ulaya umewekeza takriban EUR bilioni 3 nchini Tanzania, na kutengeneza nafasi nyingi za kazi. Umoja wa Ulaya pia unashirikiana na Tanzania, kupitia ushirikiano wa kimaendeleo na usaidizi wa bajeti.

Mazungumzo iliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Cosato D. Chumi, na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika katika Huduma ya Nje ya Umoja wa Ulaya, Balozi Rita Laranjinha. Pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam, Christine Grau, mabalozi wa Ubelgiji, Jamhuri ya Czech, Denmark, Finland, Ufaransa, Hispania, Uholanzi, Ujerumani, Slovakia, Sweden, Hungary na Italia, pamoja na Kaimu balozi wa Ubalozi wa Ireland. Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam uliwakilishwa na Kaimu Balozi Katarzyna Sobiecka. Kwa upande wa Tanzania, mazungumzo ya ushirikiano yalihudhuriwa na: Balozi Said Shaib Mussa (Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, aliyeidhinishwa pia na Poland, Hassan Iddi Mwameta, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Abouk Nyamanga, pamoja na wawakilishi wengine wa ngazi za juu ya wizara za fedha, nishati, mifugo na uvuvi, kilimo, viwanda na biashara, wizara ya maendeleo ya jamii, na wakala/taasisi za kiserikali kama Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi (NCTC), Kitengo cha Ujasusi wa Fedha (FIU) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Picha (4)

{"register":{"columns":[]}}