Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Ziara ya Rais Andrzej Duda na Mkewe nchini Tanzania mnamo Februari 8-9, 2024

09.02.2024

Mnamo Februari 8-9, 2024, Rais Andrzej Duda na Mke wa Rais Agata Kornhauser-Duda walifanya ziara rasmi nchini Tanzania, ambapo yalifanyika mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan, kutembelea Hospitali ya Aga Khan inapotekelezwa mradi kupitia Misaada ya Poland, pamoja na kushiriki katika tafrija ya wanajamii wa Poland.

President Duda in Tanzania 2024_0

Katika ziara yake, Rais Andrzej Duda alizungumza na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uwezekano wa kukuza ushirikiano na maendeleo kati ya Poland na Tanzania. Maeneo ya kuimarisha ushirikiano ni kwenye utalii, kilimo, viwanda vya kisasa, teknolojia ya habari na mawasiliano, usimamizi wa rasilimali za maji na elimu. Rais alielezea kuhusu uwezekano wa kuendeleza ushirikiano katika sekta za utalii na kilimo.

Pia alibainisha kuwa uhusiano kati ya Poland na Tanzania ni wa muda mrefu zaidi, kwa sababu watu takriban 7,000 walikuja Tanzania wakati wa Vita Kuu ya pili. Hao walikuwa ni wakimbizi wa Poland kutoka ndani ya Urusi ya Soviet walioachiliwa kutoka kwenye utumwa na Stalin. Waliokuja Tanzania walikuwa haswa wanawake na watoto kutafuta nafasi pa kuishi maisha ya amani. Watanzania wakawakaribisha, kitendo ambacho imewafanya Wapoland wawe wana shukurani sana hadi leo.

Katika ziara yao jijini Dar es Salaam, Rais na Mkewe pia walitembelea Hospitali ya Aga Khan, ambapo Shirika la Polish Aid linatekeleza mradi za misaada katika maeneo ya matibabu ya dharura na mafunzo katika nyanja hiyo kama sehemu ya mradi unaotekelezwa na shirika kutoka Poland, PCPM. Wafanyakazi kutoka Poland wanatoa mafunzo kwa wakufunzi wa afya na wafanyakazi wa afya nchini Tanzania, na pia mafunzo ya huduma ya kwanza kwa maafisa wa vikosi vya zima moto, polisi na skauti.

Rais na Mkewe pia walishiriki katika tafrija ya wanajamii wa Poland na wahitimu wa Kitanzania wa vyuo vikuu vya Poland. Katika tafrija hiyo bendi ya kimataifa ya wamishonari waliimba muziki za Poland na Tanzania. Rais alisisitiza kwamba wamisionari kutoka Poland waliweka juhudi nyingi katika kutoa huduma za kila siku kwa watu wengine na ni mabalozi bora wa Poland katika nchi za Afrika. Rais Duda, pia alisema anatarajia uwepo wa makampuni ya Poland katika sekta mbalimbali Tanzania, sio tu kwenye utalii (ambayo tayari yapo Zanzibar), bali pia kwenye sekta za digitali, ulinzi wa taarifa, utunzaji wa mazingira, ambayo kuchangia maendeleo za nchi.

Katika ziara yake nchini Tanzania, Rais Andrzej Duda aliambatana na Balozi Krzysztof Buzalski.

Mke wa Rais Agata Kornhauser-Duda alitembelea shule ya chekechea Kurasini na Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maksymilian Segerea, vyote ambavyo vinaendeshwa na wamisionari wa Poland na kuungwa mkono na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kupitia mfuko wa Polish Aid.

Picha (8)

{"register":{"columns":[]}}