Habari
-
21.06.2022Balozi msaidizi wa Jamhuri ya Poland Piotr Kruze alishiriki katika mdahalo kuhusu historia ya Vita vya Pili vya Dunia katika Chuo Kikuu cha Jordan kilichopo Morogoro na kuwasilisha maonyesho ya Wapoland wa uhamishoni waliokuwa Tanganyika.
-
17.05.2022Ubalozi wa Poland ulishiriki kikamilifu katika Maonesho ya Elimu ya Umoja wa Ulaya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ulaya nchini Tanzania yaliyoandaliwa na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya.
-
15.05.2022Mnano tarehe 9 Mei, 2022, tuliadhimisha Siku ya Ulaya jijini Dar es Salaam. Katika tafrija hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje, LiberataMulamula, Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na wageni mbalimbali, maonesho ya picha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini Tanzania na Nchi Wanachama yaliwasilishwa.
-
07.05.2022Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani za Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Me na kusoma barua kutoka kwa Waziri SzynkowskivelSęk yenye pia ujumbe wa kuwatakia kila la kheri wakazi wote wenye asili ya Kipoland waishio nchini.
-
06.04.2022Upande wa Kaskazini – Magharibi mwa Tanzania – huko Kiabakari – miradi miwili ya maendeleo iliyofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland katika mashindano ya Polish Development Aid ya 2021 na kutekelezwa na Kiabakari Foundation pamoja na Parokia ya Kikatoliki ya Kiabakari imezinduliwa.
-
25.03.2022Mnamo Machi 23, 2022, katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam, tulifurahi kusikiliza tamasha la wasanii wa Poland na Tanzania ikiwa ni sehemu ya tamasha la 2 la Pamoja Zanzibar, lililoandaliwa na Radek Bond Bednarz na kuungwa mkono na Ubalozi wetu. Balozi Buzalski alijitolea tamasha kwa ajiri ya wahasiriwa wa vita huko Ukraine.
-
21.01.2022Shukrani kwa ushiriki wa mwanaakiolojia wa Poland Maciej Grzelczyk na ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa mwaka 2021 mradi uliotekelezwa kama sehemu ya misaada ya Kipolandi yenye lengo la kuamsha na kuelimisha wakazi wa eneo la Usandawe nchini Tanzania kwa ajili ya kulinda sanaa ya miamba na urithi wa kitamaduni wa jamii ya Wasandawe umekamilika.
-
28.12.2021Tunapenda kuwafahamisha kuwa ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam utafungwa tarehe 6-7 Januari 2022.
-
28.12.2021Shukrania kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kituo cha nyaraka,ufukuzwaji na uhamisho wa Chuo Kikuu cha Pedagogical huko Cracow,wakfu wa PU “pro Univesitatis” na Wizara ya Utamaduni na Urithi wa kitaifa, makaburi mengine ya Poland nchini Tanzania yamekaratiwa.
-
09.12.2021Mwaka huu, Shukrani kwa ushiriki wa mshirika wa ndani -A.D. Views Management Ltd. na fedha zilizochangwa kama sehemu ya ushirikiano wa maendeleo wa Poland na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam, tayari takribani wasichana na wavulana 300 kutoka wilaya ya Lushoto katika milima ya Usambara kaskazini mwa Tanzania wanahudhuria vyumba vilivyopangwa maalum vinavyotoa sio tu mahali salama pa kucheza, lakini juu ya yote kujifunza.