Habari
-
06.08.2024Naibu Konseli wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Krystyna Fatyga, alipotembelea makaburi ya wakimbizi wa Poland yaliyopo Tengeru pamoja na washiriki wa Kongamano la Dunia la Kiesperanto, lililofanyika mwaka huu jijini Arusha.
-
28.06.2024Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam uliandaa uangaliaji wa pamoja za mechi za Poland katika hatua ya makundi wakati wa Mashindano ya mpira wa migu ya Ulaya.
-
03.05.2024Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Mei na kufafanua zaidi kuhusu historia ya Poland pamoja na mafanikio ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo baada ya kujiunga na Umoja wa Ulaya mnamo Mei 1, 2004. Pia, alisisitiza uimara wa mungano na Ukraine inayojihami dhidi ya mashambulizi ya Urusi huku ikipigania kujiunga na ulimwengu wa kidemokrasia.
-
01.03.2024Kama sehemu ya ushirikiano na EUNIC (Taasisi za Kitaifa za Utamaduni za Umoja wa Ulaya) nchini Tanzania, tulishiriki katika utekelezaji wa mradi wa "Viraka Freshi/Vipande Vipya", unaounga mkono vijana wabunifu wa Kitanzania katika sekta ya uzalishaji wa chapa mbalimbali na endelevu za kimitindo. Washirika waliounga mkono mradi ni mabalozi ya: Ufaransa, Hispania, Ujerumani, Italia, Ireland, Poland na Umoja wa Ulaya - EU, pamoja na mashirika ya Alliance Francaise, Goethe Institut na British Council, na pia mashirika ya ndani ya nchi kama vile Naledi Creative Center na CDEA Fashion Incubator.
-
09.02.2024Mnamo Februari 8-9, 2024, Rais Andrzej Duda na Mke wa Rais Agata Kornhauser-Duda walifanya ziara rasmi nchini Tanzania, ambapo yalifanyika mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan, kutembelea Hospitali ya Aga Khan inapotekelezwa mradi kupitia Misaada ya Poland, pamoja na kushiriki katika tafrija ya wanajamii wa Poland.
-
18.12.2023Toleo la III la Tamasha la Pamoja Zanzibar lilifanyika Desemba 8-10, 2023, ambapo tamasha za muziki tatu ziliandaliwa na Radek Bond Bednarz. Mwaka huu walishiriki familia maarufu ya muziki ya Tanzania Zawose na msanii kutoka Malawi NyaGo, kwa msaada wa Ubalozi.
-
10.12.2023Wanafunzi wa shule za sekondari, ufundi, pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea, tayari wanatumia kompyuta zilizonunuliwa mwaka huu kupitia mradi uliotekelezwa kwa pamoja na kituo hicho na Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, ukiwa umefadhiliwa na msaada wa Polish Aid.
-
09.12.2023Kama sehemu ya miradi ya maendeleo ya mwaka huu iliyofadhiliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Poland huko Dar es Salaam, kupitia mfuko wa Polish Aid, kiwanda cha kukausha matunda kinajengwa katika Milima ya Usambara. Mradi huo pia ununga mkono elimu ya ufundi kwa wanawake vijana na kusaidia kutengeneza mazingira ya kupata elimu na ujuzi, pamoja na kuchochea maendeleo ya ujasiriamali kwa kuwaongeza nafasi ya kupata ajira.
-
06.12.2023Tunaendelea kulinda mazingira na kukuza ujasiriamali katika Bonde la Kilombero na Milima ya UdzungwaBalozi Krzysztof Buzalski alitembelea maeneo ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam imekuwa ikiunga mkono shughuli za STEP, shirika lisilo la kiserikali, linaloweka jitihada ya kutengeneza mazingira ya amani baina ya watu na tembo katika Bonde la Kilombero na kuboresha ujasiriamali wa jamii za mitaa. Kipya katika mradi wa mwaka huu ni msaada wetu kwa mamlaka za Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa.