Habari
-
09.02.2025Timu ya Wanahistoria kutoka Kraków Yarejesha Hali ya Makaburi ya Poland huko KondoaMakaburi ya Kondoa yalikuwa eneo la mwisho ambapowamezikwa Wapoland nchini Tanzania linalohitaji urejesho wa kina wa hali.
-
31.01.2025Tayari tunawafahamu washindi wa Mashindano ya Mdahalo wa Vijana wa Umoja wa Ulaya, ambao watasafiri kwenda Poland kama zawadi ya ushindiUbalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam ulikuwa mshirika mkuu wa Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya ulioanzishwa na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam, fainali ambayo ilifanyika Ijumaa iliyopita, Januari 31, 2025. Washindi wa shindano hilo walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu viwili vya Tanzania: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini.
-
30.01.2025Ubalozi wa Poland jijini Dar Es Salaam kama mshirika mkuu wa mradi wa mashindano ya mdhahlo ya vijana ya Umoja wa UlayaChargée d'affaires a.i. wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam Katarzyna Sobiecka alizungumza na ‘The Chanzo’ kuhusu mahusiano ya Poland na Tanzania na ushiriki wetu katika Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya. Fedha za Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland na Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam zimewezesha washindi watatu wa juu wa Shindano la Mdahalo la Vijana wa Umoja wa Ulaya watazuru Poland mwaka huu!
-
29.01.2025Kuonyeshwa kwa Makala ya “Ambassador of Remembrance” katika Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam.Katika kuadhimisha miaka 80 ya ukombozi wa Auschwitz na maadhimisho ya 20 ya Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Maangamizi Makuu (yaani International Holocaust Remembrance Day), Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam uliandaa onyesho la makala ya Ambassador of Remembrance (Balozi wa Kumbukumbu) iliyoongozwa na Magdalena Żelasko.
-
13.12.2024Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Jakub Wiśniewski nchini TanzaniaZiara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland Jakub Wiśniewski nchini Tanzania tarehe 11-12 Desemba 2024, iliruhusu kubadilishana mawazo na wawakilishi wa mamlaka za Tanzania kuhusu uwezekano wa ushirikiano wa maendeleo, uwekezaji na biashara kati ya Poland na Tanzania. Pia ilikuwa ni fursa ya kukutana na wanufaika wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa jijini Dar es Salaam kwa mfuko ya Polish Aid.
-
10.12.2024Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa UlayaMazungumzo ya kwanza ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya chini ya Mkataba wa Samoa yalifanyika tarehe 10 Desemba 2024 jijini Dar es Salaam.
-
02.12.2024Tunaendelea na juhudi za kulinda mazingira na kukuza ujasiriamali katika Bonde la Kilombero na Milima ya Udzungwa.Konseli wa Jamhuri ya Poland, Wojciech Łysak, alitembelea eneo la mradi wa maendeleo unaoendeshwa na shirika la Southern Tanzania Elephant Program (STEP) kwa msaada wa Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam. Malengo ya msingi ya mradi ni kukuza kuishi pamoja kwa amani kati ya binadamu na tembo katika bonde la Kilombero na kuimarisha maisha ya wajasiriamali wa ndani. Mpango huo unafadhiliwa na mfuko wa Polish Aid.
-
02.12.2024“Feast of Fire” kwenye tamasha la filamu la “ZIFF Goes Mainland”Kama sehemu ya toleo la 2024 la Tamasha la Filamu la "ZIFF Goes Mainland", lililofanyika kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 21, 2024, filamu kutoka nchi za Afrika na mataifa kumi ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na Poland na Ukraine, ziliwasilishwa.
-
29.11.2024Siku ya Uhuru wa Poland nchini TanzaniaNovemba 8, ubalozi wetu ulikuwa na sherehe ya kuadhimisha miaka 106 ya Poland kupata uhuru wake. Tuliwakaribisha Wapolandi waishio Tanzania na watanzania waliohitimu vyuo mbalimabali Poland kujumuika nasi katika maadhimisho hayo.
-
29.11.2024Tunaunga mkono juhudi za kurudisha msitu wa hifadhil wa MagomberaKonseli wa Jamhuri ya Poland Wojciech Łysak alitembelea maeneo yenye miradi ya maendeleo yanayoungwa mkono na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa mfuko wa Polish Aid katika msitu wa Magombera